KUNA KUSOMA KWELI KATIKA SEKONDARI YA CHINI ?

 Naam, ni muhula mwingine wa pili, tangu kuanzishwa rasmi kwa sekondari ya kiwango cha chini. Jambo ambalo wakenya walilikumbatia kwa hisia changamano ; Wapo waliodai kwamba mfumo mzima wa Mtalaa wa umilisi hauna mwelekeo na ni mfumo ghali kuweza kumudiwa na Serekali ya Kenya, hadi wakataka utupiliwe mbali, 

Vilevile wapo wengine wengine ambao waliuona mtalaa wa umilisi kama suluhisho kamili kwa matatizo yanayokumba nchi kama vile ukosefu wa ajira kutokana na mfumo wa 8.4.4 ambao uliwandaa wanafunzi kuajiriwa tu.
Serikali nayo imesalia kidedea kuhakikisha kuwa mtalaa huu wa umilisi unafanikishwa.
Ila maswali ambayo wazazi wengi wanajiuliza  iwapo wanao ni kweli wanasoma au ni kupoteza muda tu? Hii inatokana na imani yao kuendelea kudidimia kutokana na changamoto zinazoukabili mfumo huu wa elimu. Baadhi ya changamoto hizi ni : Shule nyingi za Sekondari ya Chini , ziliweza kupokea tu mwalimu mmoja kwa kila shule, katika mpango mzima wa serikali wa kuwaajiri walimu elfu thelathini, Hata hivyo walimu wenyewe walipewa jukumu la kufundisha masomo yote , bila ya kujali eneo analozamia mwalimu.
Mwalimu wa Historia anafundisha sayansi na hata hisabati,  wasiwasi uliopo ni kuwa , kuna uhakika upi kuwa mwalimu huyu mmoja anamudu masomo haya yote na kuweza kumfikia kila mwanafunzi?
Licha ya kuwa mtalaa huu unamwondolea mwalimu jukumu la kuwa kitovu cha maarifa na kumfanya mwelekezi tu huku mwanafunzi akiwa ndiye mvumbuzi  lakini  bado ni swala ambalo lina dukuduku, kwani Vyuo vingi nchini bado pia vinaonekana kuendelea kuwafunza walimu kupitia mfumo wa zamani , na hivyo kuwafanya waendelee kutumia mbinu za kufundisha za mtalaa wa awali huku wakihitajika kutumia mbinu za mtalaa wa umilisi ambazo zinampa mwanafunzi kipau mbele.
Aidha wakenya wengi wamelalamikia swala nzima huku wakidai kuwa wanao wa gredi ya saba wamekuwa wakiketi tu shuleni bila ya kufundishwa kutokana na changamoto hizi , na hivyo wana wasiwasi kuwa huenda mkondo huu ukaendelea katika muhula huu ambao umeanza , hivyo kupelekea wanafunzi hao kuendelea kupotezewa muda.
Hata hivyo rais wa Kenya Daktari William Samoei Ruto, amejitokeza waziwazi katika mahojiano aliyoyafanya na vyombo vya habari hapo jana nikumnukuu "Serikali imo mbioni kuhakikisha kwamba mtalaa wa umilisi unafakiwa, kwa hiyo ina mpango wa kuajiri walimu alfu thelathini na tano katika makadirio ya bajeti ya mwaka 2023/2024"
Hii itawapa afueni walimu wa sekondari ya chini kwa kuongeza idadi ya walimu. 
Hata hivyo hivyo ni vyema wananchi waelewe kuwa mfumo huu upo katika hatua za kuzinduliwa na haujashika njia hivyo lazima changamoto ziwepo. Kwani ukiona vyaelea jua vimeundwa na ni wakati wa ujenzi, Shabaash.

Mwaandishi: Jairus Mafunga
Lakabu : Jaystar

Maoni