Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2023

KUNA KUSOMA KWELI KATIKA SEKONDARI YA CHINI ?

  Naam, ni muhula mwingine wa pili, tangu kuanzishwa rasmi kwa sekondari ya kiwango cha chini. Jambo ambalo wakenya walilikumbatia kwa hisia changamano ; Wapo waliodai kwamba mfumo mzima wa Mtalaa wa umilisi hauna mwelekeo na ni mfumo ghali kuweza kumudiwa na Serekali ya Kenya, hadi wakataka utupiliwe mbali,  Vilevile wapo wengine wengine ambao waliuona mtalaa wa umilisi kama suluhisho kamili kwa matatizo yanayokumba nchi kama vile ukosefu wa ajira kutokana na mfumo wa 8.4.4 ambao uliwandaa wanafunzi kuajiriwa tu. Serikali nayo imesalia kidedea kuhakikisha kuwa mtalaa huu wa umilisi unafanikishwa. Ila maswali ambayo wazazi wengi wanajiuliza  iwapo wanao ni kweli wanasoma au ni kupoteza muda tu? Hii inatokana na imani yao kuendelea kudidimia kutokana na changamoto zinazoukabili mfumo huu wa elimu. Baadhi ya changamoto hizi ni : Shule nyingi za Sekondari ya Chini , ziliweza kupokea tu mwalimu mmoja kwa kila shule, katika mpango mzima wa serikali wa kuwaajiri walimu elfu the...